Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia ajali ya Basi la abiria Kampuni ya Batco, lenye namba za usajili T608 DMP linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mahaha Wilayani Magu.

Basi hilo linadaiwa kusombwa na maji mapema asubuhi ya leo Desemba 13, 2023 wakati dereva akijaribu kuvuka Daraja la Mto Simiyu.

Afisa Habari wa wilaya ya Magu amekiri kutokea kwa ajali hiyo ambapo wakati akihojiwa mapema hii leo alidai Uongozi upo njiani kuelekea eneo la tukio.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa basi ambaye alilazimisha kuvuka bila tahadhari huku akiwa amebeba abiria.

Abdelhak Benchikha amwaga sifa Simba SC
Mauricio Pochettino ashinikiza usajili Chelsea