Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’, Wallace Karia amesema Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameipa heshima Tanzania kwa kukarabati wa Uwanja wa Amaan.

Uwanja huo ulizinduliwa jana Jumatano (Desemba 27) tayari kwa kutumika katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa baada ya kufanyiwa ukarabati.

Akizungumzia uwanja huo, Rais Karia alimpongeza Dk Mwinyi kwa kile alichokitanya.

“Hili la kuhakikisha Uwanja wa Amani na Gombani vinakarabatiwa katika viwango ambavyo vinakidhi ni jambo kubwa na tunamuombea Mwenyezi Mungu, Dk Mwinyi aweze kumpa maono na afya njema azidi kutufanyia mengi katika nchi yetu,” amesema.

Ameongeza: “Hili ni jambo limetuheshimisha sisi na ukiona kwenye mitandao ya mpira duniani Uwanja wa Amaan ni gumzo, hili tukio inabidi tulienzi na ndio maana tumebadilisha ratiba za ligi, kambi za timu ya taifa kwa ajili ya AFCON 2023 ili tuweze kuenzi jitihada zilizofanyinywa na kiogozi wetu.”

Rais Karia amesema kwa sasa kuna viwanja viwili, cha Benjamin Mkapa na Amani ambavyo vinaweza kutumika katika mashindano yoyote. Akisema Rais Samia Suluhu Hassan pia, alitoa maelekezo uwanja wa Dodoma na Arusha na vya majiji kuwa katika hali nzuri.

Amesema jitihada anazofanya ni katika kuhakikisha vijana wanacheza katika viwanja rafiki na kuweza kufanya vizuri zaidi na kuwaepusha na ajali mbalimbali za kimichezo zinazosababishwa na uwanja.

Amesema kuna viwanja vingine viwili vya mazoezi na vingine Dar es salaam vitakarabatiwa.

Kocha Asec Mimosas abariki usajili wa Karamonko
Mfahamu Samaki anayetumia Umeme kuwinda, kujilinda