Moja ya viumbe hai ambavyo vinaweza kukuachia maswali kiasi ukakosa majibu halisi ni Samaki anayeitwa Electric Eel. huyu alipewa jina hilo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzalisha umeme mpaka kufikia kiasi cha Volts 650.

Umeme wanaozalisha hutumia kama silaha katika Mawindo yao na pia kama ulinzi shirikishi pindi wanaposhambuliwa.

Uzalishaji wa Umeme

Uzalishaji wa umeme wa Samaki huyu huwa ni kwaajili ya kukamata mawindo yake ambapo kwa kutumia nguvu hiyo ya Umeme, hupiga shoti windo lake na kumfanya kubaki katika eneo hilo hilo
akiweweseka kwa dakika zake za mwisho na kisha kumfanya chakula.

Kuhusu Ulinzi, huzalisha umeme ili kama atashambuliwa basi umeme humtetemesha kiumbe anayetaka kumdhuru, lakini swali muhimu la kujiuliza ni je, uwezo huo wa kuzalisha umeme wanaupata wapi?

Uwezo wake wa kuzalisha umeme, ni kutokana na kuwa na baadhi ya ogani maalumu ambazo hutoa umeme, zilizoundwa na seli zaidi ya 6,000 ambazo ndizo huzalisha umeme pindi anapohitaji kutumia kwa shughuli zake.

Wanakopatikana.

Samaki hawa hupatikana katika mifereji kadhaa na baadhi ya mito kutoka msitu wa Amazon huko Amerika ya Kusini na tabia zao ni kwamba wao mchana hawaoni vizuri, hivyo mawindo yao kwa asilimia kubwa hufanya usiku.

Lakini pia, kwa kila baada ya dakika kadhaa ni lazima waje juu kidogo kwa ajili ya kupumua sababu wao hawana mapezi yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza Oksijeni ya kuwasaidia kupumua ndani ya maji.

Hata hivyo, wao wana tabia pia ya kuzalisha umeme kiasi kidogo kama Volts 10, ambazo hutumia kama
rada kwaajili ya kujua mawindo yake yapo wapi pia humsaidia kwa usafiri wake na kuhisi adui anayemnyemelea.

Kuua Binadamu.

Vifo vya binadamu vilivyowahi kutokana na Samaki huyu ni vichache sana kuwahi kutokea, lakini ukimshika jiandae kupigwa na shoti moja matata sana.

Kwa hapa kwetu barani Afrika kuna Samaki wanaitwa Knifefish, wao wana utaratibu unaokaribia kufanana na huyu Samaki aina ya 

Wallace Karia ampongeza Rais Hussein Mwinyi
BFT kutangaza timu ya Taifa