Lydia Mollel – Dar es Salaam.
Ili kutokomeza uuzaji na utumiaji wa Dawa za kulevya, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam, imehaidi kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania – DCEA.
Kauli hiyo, imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila na kusema operesheni hiyo ni endelevu na hakuna yoyote atakae onewa bali watakamata kwa ushahidi husika.
Amesema, “Kamaishna Jeneral amenieleza na kunidhibitishia kwamba hakuna mtu yoyote atakayeonewa na kwamba kila mmoja atakae kamatwa hatakamatwa kwa ushahidi wa yeye kuhusika au yeye kuwa mnunuzi au yeye kuwa muuzaji wa dawa za kulevya.”
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema Vita ya dawa za kulevya kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kubwa na watashirikiana na DCEA ili kuvunja mtandao wa Dawa hizo.
Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania-DCEA, Aretas Lymo alimshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kuwatia nguvu ya kuendelea kufanya operesheni hiyo inayoendelea Nchini.