Wakati kikosi cha Simba Sc kikijiandaa na safari ya kuelekea visiwani Zanzibar, tayari kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024, Kocha Abdilhak Benchikha amesema atahakikisha ataendelea kutoa nafasi kwa wachezaji wanaojituma uwanjani na siyo kuangalia majina majina maarufu.
Simba SC itashuka dimbani Jumatatu (Januari Mosi) katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya JKU utakaochezwa katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar kuanzia 2:15 usiku.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Kocha Benchikha amesema anataka kuona kila mchezaji anatimiza makumu yake uwanjani na hataangalia majina makubwa katika michuano yote watanayoshiriki.
Benchikha amesema yeye ni kocha mwenye kusimamia misingi na kuamini kile kinachofanywa na mchezaji uwanjani bila kujali majina makubwa.
“Nitaendelea kusimamia kauli yangu ya kutoangalia jina la mchezaji, ninachotaka katika kikosi changu kila mchezaji awajibike kutimiza malengo ya timu, Simba SC ni timu kubwa na kila mchezaji ana uwezo ndiyo maana yupo hapa” amesema Benchikha.
Kocha huyo amesema siku chache ambazo amekaa na timu hiyo amebaini uwezo mkubwa wa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa hawatumiki lakini yeye atahakikisha anawajengea uwezo wa kujiamini na kufikia malengo aliyojiwekea.
Amesisitiza wanaenda katika maşhindano Kombe la Mapinduzi kuhakikisha wanapambana kupata ubingwa ikiwemo kuwasuka vyema wachezaji wake kuelekea katika michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Benchikha amewaomba viongozi na mashabiki kuendelea kumpa sapoti wanafikia yakutosha katika kuhakikisha malengo waliyojiwekea kwa pamoja.