Kocha mpya wa Ihefu. Mecky Mexime amesema kazi kubwa aliyonayo ni kuhakikisha anatoa Ihefu kwenye nafasi ya 13 iliyopo sasa.

Ihefu haijawa na matokeo mazuri msimu huu, na sasa imemchukua baada ya kutokuwa na kocha mkuu tangu alipoondoka Moses Basena ambaye alichukua nafasi ya Zubeir Katwila aliyejiunga na Mtibwa Sugar.

Maxime ambaye aliachana na Kagera Sugar hivi karibuni, atatakiwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri kwenye timu hiyo.

“Kuna wakati ugumu wa majukumu unatambulisha ubora wa mbinu za kocha, ni kweli kazi yetu ni ngumu sana, ila hatuna budi kupambana nayo kuifanya Ligi Kuu iendelee kuwa bora.

Tayari nimekabidhiwa majukumu, nahitaji kukaa na wachezaji ili kujua nianzie wapi, ili kama kutahitajika maboresho nijue mapema, kwa maana ya usajili nitafanya, kikubwa ni kuhakikisha timu inakuwa salama na kuitoa kwenye nafasi mbaya iliyopo kwa sasa.

“Kwa sasa sina maneno mengi ya kuzungumza, nipeni muda niisome timu, kisha nitawaambia nakwenda kuanza na kitu gani,”amesema kocha huyo mzoefu wa Ligi Kuu Bara.

Mbombo anaondoka Azam FC
Benchika kumpa changamoto Tshabalala