Afara Suleiman – Manyara.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kupeleka magari Matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance) na kujenga kituo cha Afya katika eneo lililotengwa kwa makazi ya watu Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, kufuatia uharibifu wa maporomoko yaliyosababishwa na mafuriko.
Waziri Ummy ameyasema hayo kufuatia ziara yake aliyoambatana na timu kutoka Wizara ya Afya, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ya kutembelea eneo lililoathirika na mafuriko hayo yaliyopelekea vifo vya watu 89 na majeruhi 139.
Pia ametembelea na kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Vituo vya Afya, Zahanati na kuzungumza na watumishi wa Afya pamoja kuwajulia hali majeruhi Watano wa mafuriko wanaondelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga amesema wataalam wa afya wamefanikwa kidhibiti magonjwa ya mlipuko na kutoa elimu kwa Wananchi na waathiiriwa wa mafuriko hayo.