Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.

Wanawake wa Baraza kuu la Wanawake wa Kiislam Tanzania Mkoa Manyara, wamefika katika mji wa Katesh Wilayani Hanang kutoa mkono wa pole kwa Wanawake wenzao wa kiislam waliondokewa na wenza wao katika mafuriko yaliyotokea Desemba 3, 2023.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Mkoa, Zainab Sige amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kusikia wapo Wanawake wa Kiislam ambao wamefiwa na waumezao hivyo kwa mujibu wa dini hiyo wanapaswa kukaa Eda na waliamua kijichangisha kununua vitu mbalimbali ili kuwafariji.

Wanawake waliopata msaada huo ni Khadija Said, ambaye amefiwa na mume wake na watoto wawili na mwili wa mtoto mmoja hajaupata mpaka akisema wakati mafuriko yanatokea yeye alikuwa safari na asubuhi ya tukio alimpigia simu mume wake Kwa ajili ya kumsalimia na watoto lakini simu hazikupatika.

Anasema baadae alipigiwa simu na shemeji yake na kupewa taarifa za tukio hilo na kuwa mume wake na watoto wawili tayari wameshafariki na mtoto mmoja ameokolewa na kwamba alikuwa Hospitali.

Khadija amesema kwasasa mtoto huyo aliyebaki anaendelea vizuri na kuishukuru Serikali, mashirika, Taasisi na Baraza hilo la Wanawake kwa kufika kumuona na na kumfariji na kumpatia msaada ikiwemo chakula na mavazi.

Adel Amrouche: Kufanya mchujo sio kazi rahisi
Miaka 30 jela kwa kumnajisi mtoto wa kambo