Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na Wanaharakati wamewaomba wanasiasa wa vyama nchini Congo kushikamana baada ya tume huru ya uchaguzi CENI kumtangaza Rais  Felix Tshisekedi mshindi wa uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba.

Wachambuzi na Wanaharakati hao, wamewataka wanasiasa wanaopinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa siku ya Jumapili Desemba 31, 2023 kuwasilisha malalamiko yao Mahakamani badala ya kuitisha maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu.

Hata hivyo, Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, ambapo Rais Felix Tshisekedi alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo, wakati wapinzani wakiendelea kulalamikia  mapungufu ya uchaguzi.

Upinzani Nchini humo, sasa una siku mbili za kuwasilisha malalamiko Mahakamani huku salama ukiimarishwa katika maeneo mbalimbali yanayotishiwa na kundi la uasi la M23 pamoja na tishio la Waandamanaji.

Makala: Afrika inavyoisubiri shida ili ipate maarifa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 2, 2024