Klabu ya Manchester United inadaiwa kuamua kutoboresha mkataba wa beki wao kutoka nchini Ufaransa, Raphael Varane kwa mwaka mmoja zaidi.

Katika mkataba wake kulikuwa na kipengele kinachoiruhusu Man United kuuboresha kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa wangehitaji kufanya hivyo.

Mbali ya mkataba wake kumalizika mwakani, mabosi wa Man United wanadaiwa kumruhusu Beki huyo kuondoka mwisho wa msimu huu ikiwa atapata timu iliyo tayari kumsajili.

Kitendo hiki kinampa ruhusa Beki huyu wa zamani wa Real Madrid kufanya mazungumzo na kusaini mkataba wa awali na timu yoyote ile ya nje ya England.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kwamba Real Madrid inafikiria kumurudisha tena beki huyu ambaye bado anatamani kucheza soka la kiushindani.

Mbali ya Madrid baadhi ya timu kutoka Saudi Arabia zilihusishwa naye lakini Varane mwenyewe anadaiwa kuwa bado anatamani kucheza soka Barani Ulaya.

Mbivu na mbichi kujulikana Simba SC
Kocha Taifa Stars awatabiria makubwa wachezaji wake