Abel Paul, Jeshi la Polisi – Mbeya.

Jeshi la Polisi limesema Mtuhumiwa Lucas Tarimo aliyekamatwa Desemba 31, 2023 kwa tuhuma za kumchoma visu na kumsababisha kifo Beatrice Minja amefariki dunia hii leo Januari 2, 2024 Wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msadizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema mtuhumiwa huyo amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kunywa sumu ya kuuwa wadudu wakati alipohisi kufikiwa na Mkono wa sheria.

Lucas Tarimo, alikamatwa akiwa Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha akijaribu kujiua kwa kunywa sumu hiyo ya kuulia wadudu, lakini Polisi walifanikiwa kumuwahi na kumkimbiza kituo cha afya ili apate matibabu.

Alikuwa akituhumiwa kumuuwa Beatrice James Minja, mauaji ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, Novemba 12, 2023 kisha kukimbia.

Ajali ya Boti Ziwa Victoria yauwa wawili
Aliyemchoma Kisu Mwanasiasa wa Upinzani adakwa