Ujazaji wa mizigo kupindukia katika Boti mbili zinazofanya safari zake Ziwa Victoria, umesababisha vifo vya watu wawili usiku wa kuamkia hii leo Januari 2, 2024 baada ya Vyombo hivyo kuzama.

Polisi Nchini Uganda, imethibitisha vifo hivyo na kusema vyanzo vya ajali hizo mbili ni hali mbaya ya hewa pamoja kubeba shehena za Mkaa na Samaki kupindukia.

Hata hivyo, makundi ya wavuvi yanadaiwa kuendelea kutafuta miili ya watu wengine ambao wanadhaniwa walikuwa abiria kwenye boti hizo, zilizokuwa zinasafirsha bidhaa kutoka visiwani kuelelekea fukwe jirani na mji wa Masaka.

Aidha, inaarifiwa kuwa watu watano walionusurika katika mikasa hiyo walisaidiwa na wavuvi na wanavijiji ambapo Matukio ya vifo vya maji hutokea kwenye ziwa hilo hasa katika vipindi wa hali mbaya ya hewa, huku wasafiri wengi wakidaiwa kupuuza matumizi ya vifaa vya usalama.

 

Zifahamu sababu za kutofikia maazimio ya mwaka
Mtuhumiwa mauaji ya Beatrice afariki dunia