Kila mwaka, mamilioni ya watu hufanya maazimio ya Mwaka Mpya, wakitumaini kufanya mabadiliko chanya katika maisha yao. Kufanya maazimio au kuweka malengo, ni kama kujiwekea muongozo wako binafsi kuhakikisha umefanikiwa.

Ulishawahi jiuliza kwanini inakuwa ni changamoto kwa wengi kutimiza malengo waliojiwekea wenyewe?

Zifahamu sababu za kutofikia maazimio ya mwaka mpya

  • Kuweka maazimio yasiyo ya kweli

Azimio ni kuhusu kile ambacho ungependa kufanya badala ya kile unachopaswa kufanya, watu hujiwekea malengo magumu kupita kiasi ambayo hayafikiki haraka, au huweka malengo rahisi kiasi ambacho huchoshwa nayo wenyewe, hivyo ni muhimu kukagua maazimio yako ili kuona kama yanaweza kufikiwa na inawezekana kuyafanikisha ndani ya muda ulioweka?

Kumbuka kwamba ili kuweka azimio, lazima ubadili tabia yako, kwa hivyo hakikisha malengo yako ni ya kuridhisha.

  • Hakuna ufuatiliaji

Ukaguzi wa kila wiki au baada ya wiki mbili hukuruhusu kufuatilia maendeleo yako na kubadilisha visingizio kuwa fursa. Kinachopimwa kinafanyika, na kile kinachofanyika kinaweza kuboreshwa na kufanywa mazoea kwa usaidizi wa mfumo mzuri wa ufuatiliaji.

Vizuizi vingi vinavyoonekana vinatokana na mawazo, makisio, hukumu, kufikiria kupita kiasi, na marejeleo ya hapo awali.Rekodi ya mafanikio husaidia katika kuhakikisha azimio linakuwa endelevu.

  • Ukosefu wa uwajibikaji

Kufanya kazi na kocha, mshauri, au mshirika wa uwajibikaji kunasaidia kuhakikisha unapata nguvu na msukumo ufaao ili kukuwezesha kuwa na ari zaidi na hata kutimiza ndoto kubwa mno.

Kwa sababu mafanikio ni jambo la muda, tunaweza kuwa na uhakika kwamba tukifuata hatua, tutafikia malengo yetu.

Epuka watu wanaokukatisha tamaa unapochagua mwenzi wako wa uwajibikaji, na badala yake fanya kazi na watu wanaokuinua na kukutia moyo, haswa unapojihisi chini.

Ni bora zaidi ikiwa utapanga hatua za utekelezaji kuzunguka azimio lako, uyagawanye katika sehemu ndogo ndogo, na uyapange kwenye kalenda. Malengo ya kila wiki na mipango huleta hisia ya kufanikiwa badala ya kuahirisha.

Upangaji pia huhakikisha kuwa marekebisho yote muhimu yamenakiliwa kabla ya wakati, pamoja na uelewa wa changamoto zinazowezekana kutokea. Hii inaongeza fursa yako ya kufanikiwa, haswa linapokuja suala la malengo ya muda mrefu.

  • Kutojiamini

Usiruhusu makosa yako ya zamani kuamuru maisha yako ya baadaye, baada ya kujifunza kutokana na kushindwa kwako, ni wakati wa kufanya kazi.

Kila ushindi mdogo unapaswa kusherehekewa kwa sababu inakupa motisha kufanya kazi kwa bidii ili upate mafanikio makubwa zaidi.

Kujikosoa au kuwa na mashaka hakusaidii kwa sababu inalenga umakini na nguvu zako zote kwenye “kwa nini siwezi kufanya hivi?”

Unapoboreka, jizoeshe kujihurumia na kujipenda, na usiruhusu kushindwa au kukatishwa tamaa kidogo kugeuka kuwa kushindwa kwa kudumu. Haijalishi unahisi uzito kiasi gani, jifundishe kujitia moyo na kuendelea.

Watu wengi wanashindwa kufikia malengo yao kwa sababu malengo  yao hayajulikani. Unaweza kujua unachotaka, lakini huweza kujua jinsi ya kukipata hadi utakapojua kwa nini unakitaka.

Kwa hivyo, kwa nini unafanya maazimio haya? Ni swali muhimu unalotakiwa kujiuliza kabla ya kujiwekea malengo.

Ni muhimu kuzingatia, kuchukua jukumu, kujitolea na kuelekeza umakini wote ikiwemo nguvu, mawazo na hatua ili kushikamana na maazimio ya mwaka mpya.

Kumbuka, washindi na walioshindwa wana malengo sawa; ni kile mtu anachofanya ili kujaza ‘pengo’ ndicho kinacholeta tofauti kubwa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 3, 2024
Ajali ya Boti Ziwa Victoria yauwa wawili