Rais wa Urusi, Vladmir Putin yupo nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku mbili akiendeleza mazungumzo na mwenyeji wake Rais Xi Jinping ambaye amesema ana matumaini ya kurejea kwa amani barani Ulaya na kwamba China itahakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Kwa mujibu wa Mtaalamu wa Masomo ya Kimkakati na ulinzi, Matthew Sussex amesema Putin na Xi wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuangazia masuala ya usalama wa ulimwengu na wa kikanda katika safari yake hiyo ya kwanza katika muhula wake wa tano kama rais.

Hata hivyo, Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema Putin anataka kuthibitisha uungaji mkono wa China kwa Urusi, hasa uhusiano wake wa kiuchumi na mtiririko wa vifaa vya teknolojia ambayo ni muhimu kwa juhudi za vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Naye Mtaalamu kutoka Taasisi ya Kitaalam ya Jumuiya ya Asia, Phillip Ivanov anasema Xi anaweza pia kuhitaji maelezo kutoka kwa Putin juu ya upi mkakati wa Urusi nchini Ukraine na pia hakikisho kwamba hatatekeleza vitisho vya nyuklia ambavyo alitoa hapo awali.

Ashley Cole kupewa dili England
Shirika la Posta lajipanga kutumia Magari ya umeme