Johansen Buberwa – Kagera.

Mabinti katika Halmashauri sita za Mkoani Kagera wanatarajiwa kujengewa uwezo wa kupambana na athari za Mimba za utotoni pamoja na hedhi salama, ili kufikia ndoto zao ikiwemo za kuwa Viongozi bora wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Rafiki wa Binti, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Viva Foundation, Gasper Edimund amesema lengo la mafunzo hayo ni  kumjengea Binti wa Mwafrika wa Nchi ya Tanzania kuwa nauwezo wa kujiamini na kusoma kwa uhuru.

Kwa upande wake mgeni rasmi, Afisa Tawala Wilaya Bukoba, Ajesy Katumwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwasa amesema Binti ni hazina ya Taifa na jamii na kwamba Serikali ina kazi kubwa ya kuendelea kutoa elimu ya kijinsia, kisiasa na kiuchumi ili kumkomboa mtoto wa kike.

Hafla hiyo, imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kisiasa, wawakilishi toka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini, Idara ya Elimu na dawati la jinsia ambapo kwa pamoja wamesema jamii inatakiwa kuwa na hofu ya Mungu.

Aidha, wamesisitiza juu ya suala la kujitambua kwa mabinti na kuomba ufanyike uchunguzi kuanzia shule za msingi hadi sekondari kusaidia kupunguza mabadiliko vitendo hatarishi kwa jinsia hiyo ambayo ni hazina kwa Taifa.

Kocha Azam FC amwagia sifa Navarro
Mwakinyo: Rais Mwinyi apewe heshima yake