Viongozi wa Dini kutoka Nchini Kenya, wakiongoza na Pastor Ezekel Odero wamekabidhi vifaa vya Ujenzi vyenye thamani ya Mil.11 za Kenya sawa na Mil.158 za Tanzania, vitakavyotumika kujengea Makazi ya Wananchi waliopoteza nyumba zao katika tukio la Mafuriko wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.

Misaada hiyo, mbao 14420 na Bati 1441 na itatumika kupaua Nyumba zaidi ya 100 na kuezeka Kituo cha Afya Wareta, eneo ambalo watapatiwa waathirika wa tukio la Mafuriko hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ amesema Misaada ya vifaa vya Ujenzi Vitasadia katika kukamisha Ujenzi wa nyumba za wathirika na kuwashukuru Viongozi wa Dini kwa upendo wao wakujitoa.

Mapema wiki hii, Mwenyekiti wa Mitume na Manabii Mkoa Manyara, Nabii Faraja Lucas akiongozana na manabii wengine kutoka katika maeneo mbalimbali, pia walifika Kijijini Ngendabi Katesh Wilayani Hanang’ kujionea madhara yaliyotokana na maporomoko ya tope, Mawe na Maji yaliyo tokea Desemba 3, 2023 na kufanya maombi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 4, 2024
Benchikha achimba mkwara wa mwisho