Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani – IPU na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, anashiriki Mkutano wa 27 wa Maspika na Makatibu wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini Uganda.

Mkutano huo unatarajiwa kuangazia na kutoa fursa kwa Viongozi wa Mihimili kupeana uzoefu na mbinu chanya mpya juu ya hatua mbalimbali za uendeshaji wa Mabunge.

Aidha, mkutano huo pia utaangazia namna ya  kujenga mahusiano mazuri zaidi yatakayoleta hamasa kwenye kufikia diplomasia ya Kibunge ndani ya Jumuiya hiyo.

Rais mstaafu afikishwa Mahakamani kwa uhaini
Jamii yahimizwa kuwakumbuka Wazee mahitaji maalum