Wakazi wa Mkoa wa Songwe, wametakiwa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuwafariji na kuwaweka karibu na jamii.

Kauli hiyo, imetolewa na Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Songwe, Mrakibu wa Polisi William Nyamakomago katika hafla iliyoandaliwa na kikundi cha kuwasaidia watu wenye uhitaji maalumu, kiitwacho African Genius Foundation tawi la Songwe.

Alisema, suala la malezi bora kwa wajukuu wanaoishi na wazee na kuwataka wazee hao kuwafundisha mila na desturi za Kitanzania ili kuzuia mmomonyoko wa maadili kwa watoto kwa lengo la kujenga taifa imara linalokemea na kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu kwa maendeleo ya nchi.

Aidha, SPhttps://dar24.com/250915-2/ Nyamakongo aliwaomba Wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji maalum kama kilivyofanya kikundi cha African Genius Foundation kwani kufanya hivyo ni neema kwa Mwenyezi Mungu.

Naye Mhamasishaji na Mratibu wa kikundi hicho Mkoa wa Songwe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sadam Kitembe alisema katika kikundi hicho wamejiwekea utaratibu wa kuwasaidia watu wenye uhitaji maalumu kama yatima, wajane, wazee na watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Kwa upande wa wazee hao, wamelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa elimu waliyoipata na wameahidi kutoa ushirikiano katika kila jambo linalohusu uhalifu, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto, ili kuwa na jamii bora iliyo na kizazi imara.

Katika halfa hiyo wazee hao walipata nafasi ya kushiriki chakula cha mchana na viongozi wa kikundi hicho na kupatiwa mahitaji mbalimbali kama sabuni, mchele, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupakaa, sukari, chumvi pamoja na mavazi.

 

Dkt. Tulia aongoza hamasa ufikiaji Demokrasia ya Kibunge
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 4, 2024