Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma amefikishwa mbele ya Mahakama kujibu mashtaka ya uhaini akidaiwa kujihusisha na jaribio la mapinduzi mwishoni mwa Novemba 2023.

Koroma aliyekuwa Rais kati ya 2007 na 2018, alihojiwa na Polisi mara tatu kabla ya kufunguliwa mashtaka ya mashambulizi ya silaha katika kambi ya jeshi na Gereza, jijini Freetown.

Katika shambulizi hilo, inadaiwa Wafungwa 2,000 walitoroka, miongoni mwao wakiwa ni watuhumiwa waliohusishwa na mapinduzi hayo.

Hata hivyo, tayari zaidi ya watu 50 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na binti wa Mstaafu Koroma.

Mapato chanzo anguko la Uongozi Mnada wa Pugu
Dkt. Tulia aongoza hamasa ufikiaji Demokrasia ya Kibunge