Mkuu wa Polisi Nchini Sierra Leone, Fayia Sellu amesema maelezo aliyoandikisha kwa hiyari yake Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma yanaonesha moja kwa moja kuwa alishiriki jaribio la mapinduzi la Novemba 2023.

Koroma ni miongoni mwa watuhumiwa wa kile Serikali ya nchi hiyo inachodai walihusika na jaribio la mapinduzi la mwezi uliopita na alikuwa kwenye kizuizi Nyumbani kwake wakati akifanyiwa mahojiano.

Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma.

Jumanne Desemba 12, 2023 Serikali kupitia Waziri wake wa Habari, Chernor Bah ilithibitisha kuwa sasa Koroma ni mtuhumiwa rasmi wa tukio hilo.

Kundi la watu wenye silaha, lilivamia Ghala la Silaha la jeshi, Kambi mbili, Jela mbili na vituo viwili vya Polisi mapema Novemba 26, ambapo kwenye makabiliano na Vyombo vya Usalama, watu 21 waliuawa.

Ugoro sehemu za siri chanzo magonjwa yasiyoambukizwa
Mafuriko: Wataalam wa Saikolojia UDSM wafika Hanang'