Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema hakuna maendeleo pasipo na amani, umoja na mshikamano wa watu.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wqkati alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Riyadhu swalihin Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema waumini hao wanatakiwa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.

Aidha, Rais Mwinyi pia amewasihi Vijana kufanya kazi za halali na kuepuka kushiriki vitendo viovu.

Chama ngoma ngumu Simba SC
Makala: Mwamba wa 'The God Must Be Crazy' aliamka