Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, Godfrey Rwekiti, amemhukumu kwenda jela miaka 20 mkazi wa Kijiji cha Sakasaka 20 Peter Ndekeja kwa kosa la kupatikana na Nyara za Serikali vipande viwili vya Meno ya Tembo kinyume cha Sheria.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mwalimu Mvoi aliieleza Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 29, 2023 katika Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Meatu.
Aidha, katikq hatua nyingine pia Mahakama hiyo pia imemhukumu kwenda jela miaka 20 Mshatikiwa Gidion Yohana, mkazi wa kijiji cha Sungu kwa kosa la kupatikana na Nyara za Serikali ambazo ni miguu minne ya Twiga.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mwalimu Mvoi mbele ya Mahakama hiyo alisema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 24, 2023 katika eneo la Isagusa lililopo ndani ya Hifadhi ya Maliasili ya kijiji cha Makao, kilichopo Wilaya ya Meatu.