Klabu ya Dodoma jiji imeanza kuzipigia hesabu mechi mbili za viporo dhidi ya Young Africans na Mashuja FC wanazoamini ni muhimu kushinda ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hadi sasa Dodoma Jiji FC ina pointi 18 kutokana na mechi 13 ilizocheza katika Ligi, huku ikiamini itazibeba pointi sita kupitia mechi hizo.

Kocha msaidizi wa Dodoma Jiji FC, Kassim Liyogope amesema kazi kubwa waliyonayo kwa sasa ni kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kupata ushindi katika mechi hizo mbili pamoja na zingine.

“Tunaridhishwa kwa kweli na ubora wa wachezaji wetu hadi sasa, ndio maana hata kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo tutaongeza tu nafasi chache zile ambazo zina mapungufu.” amesema Liyogope aliyeongeza baada ya kumaliza na Young Africans na Mashujaa watajipanga upya kujua ni namna gani wanacheza mechi 15 za duru la pili ili kusudia wamalize katika nafasi nne za juu kufikia malengo yao.

Liyogope ameweka wazi bado timu iko mapumzikoni baada ya ligi kusimama kupisha Kombe la Mapinduzi na michuano ya ‘AFCON 2023’ na watarejea mazoezi hivi karibuni.

Makala: Jinsi wachumia juani wanavyogombea kivuli
Mwangata afichua usajili wa Ndikumana