Kiungo wa zamani wa Tanzania na Pan African, Mohamed Adolf amesema anaiona kesho nzuri ya Taifa Stars kutokana na aina ya wachezaji walioteuliwa na kocha Adel Amrouche kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zitakazounguma nchini Ivory Coast.

Ridhard amesema kikosi cha Tanzania kinaundwa na nyota wengi wenye uwezo mzuri, hivyo anaona kesho nzuri ya timu hiyo kutokana na mseto wa wachezaji ambao wameonesha kuwa na kitu.

“Si kikosi kibaya, kuna wachezaji wengi ambao wana umri mdogo ambao wameonyesha kuwa tayari kwa mapambano, kama kitaendelea kupewa nafasi ya kucheza pamoja kwa muda mrefu, basi tunaenda kuwa na timu imara.

“Mpira wetu umekuwa unapiga hatua na hapa tulipofika inaonyesha kuwa tuna kesho nzuri kama misingi itaendelea kujengwa kupitia kwa vijana hawa,” amesema.

Amesema kuwa na wachezaji wanaocheza ligi mbalimbali duniani inaleta kitu kipya kwenye kikosi na kama wataendelea kutumika siku moja historia nzuri ita andikwa kwa Tanzania.

Rishard anakumbukwa kwa kufunga bao katika mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kufuzu dhidi ya Zambia, Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, mechi iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya marudiano mjini Lusaka, Tanzania ikashinda bao 1-0 na kujikatia tiketi ya kwenda Nigeria mwaka 1980.

Kupeleka Watoto Shule mwisho Januari 11 - RC Sendiga
Adebayor: Victor Osimhen akacheze EPL