Chama cha Mapinduzi – CCM, kimetoa maoni na ushauri juu ya miswada minne ya sheria Iliyosomwa kwa mara ya kwanza katika Bunge la Mwezi Novemba ikiwemo muswada wa sheria ya uchaguzi wa wabunge na madiwani wa mwaka 2023 na muswada wa Sheria ya tume ya Taifa uchaguzi wa Mwaka 2023.

Akizungumza wakati akitoa maoni juu ya maboresho ya sheria leo Januari 9, 2024 Mery Chatanda amesema CCM imepongeza kamati ya bunge, utawala katiba na sheria kwa utaratibu huo wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wanawasilisha maoni yao kwa uwazi na uhuru.

“Chama cha Mapinduzi kinampongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa kufanya maboresho ya sheria iliyopelekea miswada hiyo kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Novemba 10 mwaka 2023,” amesema.

Hata hivyo CCM pia kimeipongeza kamati ya bunge ya utawala, katiba na sheria kwa utaratibu mzuri iliyouweka wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ambao eamewasilisha na wanaendelea kuwasilisha maoni yao kwa uwazi na kwa uhuru.

Pia amesema CCM inakubaliana na mapendekezo ya vifungu vilivyowasilishwa katika miswada hiyo ikiwa ni pamoja na utaratibu uliotumika wa kuzichukua ibara za katiba kama zilivyoainishwa na kuziingiza katika miswada ya sheria.

“hizi ni njia sahihi za kuhakikisha kwamba sheria hizo hazipingani na katiba ya Nchi hivyo utaratibu huu uendelee kuzingatiwa”. Amesema Chatanda

Ameongezea kuwa, “muda unao pendekezwa katika miswada ya sheria mpya ya tume ya uchaguzi kukutana mara nne kwa mwaka na wakati wowote inapohitajika ni muhimu eneo hilo liangaliwe upya ili kupunguza gharama za uendeshaji wa chombo hicho.”

Kocha Chelsea afunguka usajili wa Henderson
Msuva avunja ukimya usajili Young Africans