Watu watatu wa familia moja akiwemo Bibi, Mama na Mjukuu wamefariki na Baba yao Sengo Hamis akijeruhiwa kufuatia Mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2024 zilizosababisha Mto Mgolole wa Manispaa ya Morogoro kufurika.

Akithibitisha kutokea kwa tulio hilo, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa Morogoro,  Shabani Marugujo amesema wamefanikiwa kuopoa miili ya watu miwili akiwemo Mjukuu Asnath (6) na bibi yake, Thelesia Adolph (70 -76).

Amesema, juhudi za kuutafuta mwili wa Mwanahamis Issa, ambaye ni mama wa familia hiyo bado zinaendelea, huku baadhi ya Wananchi wakihimizana kuchukua tahadhari na kutoyadharau maji katika kipindi hiki cha masika kilicho na Mvua kubwa.

Awali, mashuhuda walisema tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia hii leo, baada ya nyumba ya familia hiyo ilizingirwa na maji na wakati wakijaribu kujiokoa kwa kuvuka mto, maji yaliwazidi nguvu.

Wawili wasimamishwa kazi kwa ubadhirifu Kagera
Makala: Kumlalia Mamba ni Baraka, wanamuabudu