Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuwasimamisha kazi watumishi wawili kwa kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na ubadhilifu wa fedha za Serikali.

Sima ametoa agizo hilo wakati akikagua miradi ya Manispaa na kuangalia idadi ya wanafunzi walioripoti Shule ya Sekondari ya Omumwani ya Kidato cha Tano na sita.

Shule hiyo, ilipokea kiasi cha Sh. 716 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa saba na mabweni manne, ambao haujamridhisha Mkuu huyo wa Wilaya.

DC Sima amewataja majina watumishi hao kuwa ni Saraphina Rwezaura ambaye ni Mkuu wa Shule ya Omumwani na Mhasibu wa Manispaa, Christina Tibenda.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 11, 2024
Mafuriko yauwa watatu wa familia moja Moro