Wizara ya Katiba na Sheria imesema imejipanga kikamilifu kuhakikisha Wananchi wananufaika na Kampeni ya Mama Samia Legal Aid, ambayo imelenga kutoa msaada wa kisheria bure kwa jamii katika masuala ya migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi na matunzo ya Watoto.

Waziri wa Katiba na Sheria, Pindi Chana ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni hiyo katika Viwanja vya Stendi ya zamani Mkoani Singida, ambapo ameeleza kuwa msaada wa kisheria unatolewa bure katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida kuanzia Januari 11-19, 2024.

Amesema, lengo ni kufikia jumla ya Kata 70 na vijiji 210 vya mkoa wa Singida, huku akitoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa huo na maeneo jirani kuitumia vizuri fursa hiyo kwa kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu.

Uhudhuriaji wa Wanancho katika zoezi hilo utawasaidia kupata elimu na huduma za masuala mbalimbali ya kisheria zitakazotolewa bure na kuwataka viongozi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji kutoa ushirikiano.

Nzwalile amkaribisha Makonda Babati, akemea wapiga dili
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 11, 2024