Madereva wa Bajaji Wilayani Momba,  wametakiwa kuachana na kutojihusisha na vitendo vya kihalifu wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wito huo umetolewa na Polisi kata wa kata ya Chapwa, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Antony Sabasaba alipokutana na madereva hao kuwapa elimu ya madhara ya kuwaficha wahalifu Wilayani humo.

Alisema, kazi ya bajaji ni kazi kama kazi nyingine hivyo kila dereva atambue thamani yake na abiria wake kwa kumlinda mpaka afikapo na sio kumfanyia vitendo vya kihalifu kama uporaji, kumjeruhi au kumbaka, kwani kufanya hivyo ni kuichafua kazi ya usafirishaji na pia ni kosa kisheria.

Aidha, Sabasaba alisema, “Vijana hamtakiwi kufumbia macho vitendo hivyo na mnapaswa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa madereva wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria haraka ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.”

Makala: Kumlalia Mamba ni Baraka, wanamuabudu
Ataka Wazazi wawalinde Watoto umri wa balehe