Polisi Kata wa Kata ya Kimang’a iliyopo Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mlekwa amewaomba Wananchi wa Kata ya Kimang’a kuendeleza ushirikiano na Jeshi la Polisi hasa kwenye utoaji wa taarifa zenye viashiria vya uhalifu.

Mkaguzi huyo Msaidi Mlekwa ametoa ombi hilo wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo na kuwasisitiza umuhimu wa utoaji taarifa za wahalifu jinsi unavyosaidia katika kuondosha vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Unapoona kiashiria cha uhalifu toa taarifa kwenye vyombo husika ili ziweze kufanyiwa kazi, lakini niwaahidi huduma bora zitakazotolewa kituoni hapo ikiwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na wananchi,” alisema Inspekta Mlekwa.

Aidha, amesema viongozi wa Serikali za Mitaa na kata wanapaswa kushirikiana na Polisi kata kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu ili wananchi waweze kuwa salama na kuendelea na shughuli zao za Maendeleo bila kusumbuliwa na wahalifu.

Mwangata afichua usajili wa Ndikumana
Kapinga asisitiza uzalishaji Umeme wa Jotoardhi