Polisi Kata wa Kata ya Kisaki Wilaya ya Singida Mkoa wa Singida, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Gilbert Tende amewataka wazazi kutokuwa chanzo cha watoto kuacha shule kwa visingizio vya kukosa mahitaji kwani elimu ya msingi na sekondari ni bure.

Tende ameyasema hayo katika mkutano na wazazi uliofanyika kitongoji cha Irao na kuongeza kuwa hatamfumbia macho mzazi yeyote atakayeshindwa kumpeleka mtoto shule kwa kumchukulia hatua za kisheria.

“Watoto wetu kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vitendo ya ukatili wanavyofanyiwa, Hivyo kwa pamoja tushirikiane kutoa taarifa za ukatili ili watoto wetu waweze kutimiza malengo yao,” alisisiza Tende

Aidha, Tende pia amewasisitiza wananchi wa Kisaki kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wavunjivu wa amani katika kata ya Kisaki waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio kujichukulia sheria mkononi.

Makala: Hivi ni kweli Kuku alipanda Baiskeli
Vyuo vikuu wahimizwa matumizi sahihi Vifaa vya Mawasiliano