Matajiri wa Saudi Arabian, AL Etifaq hawana mpango wa kumuuza kiungo wao raia wa England, Jordan Henderson mwenye umri wa miaka 33, dirisha hili la Januari.

Taarifa hii inaibuka ikiwa ni siku kadhaa baada ya kusambaa kwa ripoti huenda nyota huyo akarejea Liverpool dirisha hili.

Henderson inataarifiwa hana furaha kwenye kikosi cha kwanza cha Ettifaq na amewaambia baadhi ya marafiki zake wa karibu alifanya makosa makubwa kwenda Saudia.

Henderson alijiunga na Ettifaq dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kuwekewa ofa nono ya mshahara wa Pauni 7O0,000 kwa juma.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na moja ya sababu zinazotajwa kumfanya atamani kuondoka ni kiwango kibovu cha timu hiyo.

Msimu huu amecheza mechi 19 za michuano yote ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo na pointi 25.

Makala: Mtafiti atafitiwa kwa mbio za Matunda
Mwijage anukia Geita Gold FC