Kwa umri ulionao sina shaka umeshawahi kushangazwa na kauli ya mtu yeyote aliyokupa na ukaitafakari ukubwa wake ama kushangaa jinsi ambavyo hukutarajia kama kiumbe huyo angeyaongea hayo, kutokana na ama umri wake au busara zake.

Wazee wa kihenga, waliwahi kukitafsiri kitendo kama hicho eti ni busara kukosea njia, sijui kama walikuwa sahihi lakini kisa hiki cha leo kinatoka kwa Mtaalamu mmoja wa masuala ya kibinadamu, aliyewahi kufanya utafiti juu ya imani ya kiutu waliyokuwa nayo waafrika, na kufanya utafiti huo kwa Vijana wadogo.

Ikafika siku moja, katika jamii fulani mtaalamu huyo akitekeleza wajibu wake, alitaka kundi hilo la Vijana waingie katika ushindani wa kukimbia akisema, mshindi wa mbio hizo angejipatia Matunda na sharti ayale peke yake.

Walimsikiliza bila kumjibu kitu, lakini vijana gawa walioerevuka walikuwa na lao moyoni na baada ya kutolewa kwa ishara ya kuanza kwa mbio, walimshangaza mtsfiki kwani Vijana hao walishikana mikono na kukimbia kwa pamoja.

Mtafiti aliwafuatilia kwa ukaribu, huku akistaajabia kitendo kile maana si kawaida katika mbio za ushindani watu wakashikana mikono na mwisho wa mbio hizo, Vijana hao waliketi kwa pamoja na kuanza kula Matunda yale kama familia moja na kwa furaha.

Mtaalamu yule aliwasogelea na kutaka kufahamu ni kwanini waliamua kukimbia kwa pamoja, ndipo mmoja wa Vijana wale akamjibu kwamba, “kama mtu angeshinda mbio zile na kupewa matunda yote ale peke yake basi hangekuwa na furaha, ilhali wenzake wote wanayo huzuni.

Alimueleza kuwa, “sisi ni wabantu, na kwetu mtu huwa vile alivyo leo kwasababu kuna watubnyuma yake wamemuandaa awe kama alivyo leo, sisi ni wamoja na tupo hivi kwavile katika maisha yetu tuliandaliwa kuwa wamoja.”

Mtafiti alibaki kinywa wazi, akitafakari kwa kina kuhusu umoja ule, maana Vijana wale waliamua kusikizana na kutenda mambo bila kubaguana.

Baadaye baada ya kutafakari kwa kina alipata pia somo na maana halisi ya utu kupitia kitendo kile, akiaminu hali ya binadamu kutenda kadiri ya hadhi yake inamfanya astahili kupata haki zote za kijamii kama elimu, afya, ajira nk.

Kwa maana nyingine, twaweza sema Mtafiti alipata kuelewa kwamba utu ni ile hali ya kutenda jambo jema kwa ajili ya mwingine bila kuwa na kinyongo, hiyana wala tarajio la kitu kutoka kwake na Vijana walimuonesha kwamba raha ya muda mfupi isiwatengenezee picha ya ubinafsi bali wabaki na umoja wao na utu wao, hapa ndugu “MTAFITI ALITAFITIWA”

Vijana vijiwe havijawahi, haviwezi kuwalipa - Sipe
Mataikun wa Saudi Arabia washtuka