Polisi Wilayani Kilosa, wamelazimika kuingia kati na kutumia busara kuwatuliza Wananchi wa Kijiji cha Kitete cha Kata ya Ruhembe Mkoani Morogoro, waliotaka kufunga Ofisi ya Mwenyekiti wa Kijiji wakidai hawataki kuongozwa nae kwa madai amekuwa hawasomei mapato na matumizi ya Kijiji kwa muda mrefu.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Flora Shayo ambaye ni Polisi Kata wa Kata hiyo amesema, amelazimika kutoa katazo hilo, ili kurudisha amani katika eneo hilo iliyoanza kutoweka, kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu.
Aliwataka wananchi hao Kutii Mamlaka zilizowekwa na Serikali na kuheshimu Sheria za nchi, lakini pia wafuate utaratibu rasmi kutatua changamoto zao hali iliyoleta maelewano na Wananchi hao kuyawany8kq huku wakiahidi kutafuta suluhu kwa njia rafiki.
Mmoja wa Wananchi hao (Jina linahifadhiwa), alisema busara za Afande Shayo zimesaidia kutuliza hasira zao na kupelekea kusitisha zoezi la ufungaji wa ofisi na kwamba watafuata ushauri wake wa wakutojichukulia sheria mkononi.