Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans, Hersi Said amesema baada ya kukosa nafasi msimu wa 2022/23, klabu hiyo itakuwa sehemu ya timu 24 zitakazoshiriki michuano ya African Football League ‘AFL’ mwaka huu 2024.

Young Africans ambao wanafainali wa Kombe la Shirikisho walikosa nafasi ya kucheza michuano ya ‘AFL’ ambapo ukanda wa CECAFA uliwakilishwa na Simba SC ambao wako ndani ya timu 10 bora Barani Afrika kwa sasa.

Michuano hiyo ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza Barani Afrika na kuzinduliwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, ilishirikisha timu nane ambazo ni Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia na Wydad kutoka Morocoo hizi zikitoka Kanda ya Kaskazini.

Enyimba ya Nigeria na Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutoka Ukanda wa Kati-Magharibi huku Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini, Petro Atletico ya Angola na Simba SC kutoka ukanda wa Kusini-Mashariki.

Amesema Young Africans waliridhia baada ya makubaliano binafsi na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, Patrice Motsepe kuwa walichokifanya mwaka jana ya kuchagua timu shiriki ni kutokana na mazingira ya wakati huo ambapo zilichukuliwa timu nane za kuanzisha Africa Football League.

“Lakini kwa kuwa walikuwa na idadi kamili ya klabu walizokuwa nazo na kwa kauli yake amenidhihirishia kuwa Young Africans itashiriki mashindano hayo mwaka huu 2024.

“Kwangu kauli hiyo inatosha na tumeipokea na hatuna sababu ya kufuatilia nini kilichotokea nyuma na tunakubaliana na maamuzi ya viongozi, tuko tayari kushiriki AFL mwaka 2024,” amesema Hersi.

Tunahitaji mageeuzi sekta ya Uchumi - Sangu
Jonesia Rukyaa, Soud Lila watupwa FIFA