Mwamuzi wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Jonesia Rukyaa na mwamuzi msaidizi Soud Lila wamevuliwa beji za FIFA baada ya kushindwa katika majaribio.

Aidha, waamuzi wengine wawili wa Tanzania, Amina Kyando kutoka Morogoro na Mary Seleman wa Dar es salaam wamepata beji za FIFA kwa mara ya kwanza baada ya kufikia vigezo vya kimataifa.

Jonesia ambaye alirudishiwa beji mwaka 2023 baada ya kutokuwa nayo kwa miaka miwili kutokana na likizo ya uzazi, pamoja na Soud walifeli mtihani wa utimamu.

Katika orodha iliyowekwa kwenye ukurasa wa FIFA, Tanzania ina waamuzi 17 kwa mwaka 2024.

Waamuzi wa kati ni sita, ambapo wawili ni wanawake na waamuzi wasaidizi wako tisa ambapo wanawake ni wanne.

Waamuzi wa kati wanaumne ni Ahmed Arajiga, Ramadhani Kayoko, Hery Sasii na Salum Nasir na wanawake ni Tatu Malogo na Amina Kyando.

Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba, Mohamed Mkono, Kassim Mpanga, Ramadhani Rajabu Ally na Hamdani Said na wasaidizi wanawake ni Janet Balama, Zawadi Yusuf, Glory Tesha na Selemani Mary.

Kwa upande wa waamuzi wa soka la ufukweni ni Jackson Msilombo na Mohamed Ally.

Young Africans kushiriki AFL 2024
PSG kumwaga fedha FC Bayern Munich