Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane ametabiri kuwa wako katika Kundi gumu katika Fainali za Mataifa ya Bara la Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoanza keshokutwa Jumamosi (Januari 13) nchini Ivory Coast.

Amesema kuwa timu za Gambia, Cameroon na Guinea ambazo wako nazo Kundi moja, sio za kuzibeza kwani zinaweza kufanya lolote na kupata matokeo.

“Mchezo dhidi ya Cameroon utakuwa mgumu sana, hivyo hatuwezi kuwadharau wapinzani wetu,” amesema mchezaji huyo bora mara mbili wa Afrika alipozungumza na waandishi wa habari.

“Wakati nakubaliana na hilo hakuna timu kati ya hizo ni nyepesi, tuna uwezo wa kucheza hatua ya mtoano,” amesema nyota huyo wa zamani wa FC Bayern Munich na Liverpool.

Senegal iliishinda Cameroon miaka 34 iliyopita katika mhezo wa hatua ya makundi huko Algeria wakati timu hizo zilipokutana kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Afrika.

Lakini Cameroon imekuwa ikipanda na kushuka tangu wakati huo, ikishinda Robo Fainali, baadae fainali ya mwaka 2002 na Robo Fainali nyingine baada ya Penati tano tano.

Senegal iliifunga Guinea mara mbili, lakini suluhu pekee kati yao katika Hatua ya Makundi miaka miwili iliyopita ikielekea kushinda taji hilo la Afrika kwa mara ya kwanza.

Morocco yaanza kujihami AFCON 2023
Tunahitaji mageeuzi sekta ya Uchumi - Sangu