Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtama iyopo Wilaya na Mkoa wa Lindi, wametakiwa kutoona kazi za mikono kuwa ni adhabu pindi wanapopangiwa kufanya kazi hizo wanapokuwa shuleni au nyumbani.
Kauli hiyo imetolewa na Polisi Kata ya Mtama, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Marwa Benedict wakati alipofika shuleni hapo kwa lengo la kutoa elimu ya ushirikishwaji Jamii.
Amesema, amefurahishwa na wanafunzi hao baada kwawakuta wanafanya shughuli za usafi wa mazingira shuleni hapo ni utaratibu wa kumjenga mwanafunzi kutambua na kujifunza kazi za mikono ili kumsaidia kwa baadaye.
Nao baadhi ya Wanafunzi wamesema wamefurahi kupata maelekezo hayo ambayo yatawasaidia katika kufanikisha safari yao kielimu.