Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limewataka Wananchi wa Kata ya Kimobwa Wilayani Kasulu, kujenga utaratibu wa kuwajali na kuwalinda Wazee kwani ni tunu na kupitia wao jamii itajifunza mambo mengi ikiwemo historia.

Hayo yamesemwa na Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Kokugonza Ally wakati akitoa elimu ya usalama wa wazee ambapo amesema wazee wamelitumikia taifa na kuleta maendeleo yanayoonekana sasa jamii inawajibu wa kuwalinda, kuwaheshimu, kuwajali na kuwapa huduma muhimu.

Kokugonza pia amesema wapo baadhi ya wananchi wanawanyanyasa kwa kuwafanyia vitendo vya ukatili wazee ikiwemo kuwatenga na jamii na kuwataja wachawi vitendo vinavyoweza kupelekee wazee kutendewa matukio ya uhalifu mfano kujeruhiwa.

Aidha, ameongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watuhumiwa wote wanaotenda matukio ya ukatili dhidi ya wazee.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 14, 2024
Wanafunzi waambiwa kazi za mikono sio adhabu