Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Pwani, Omary Punzi kwa niba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Taifa, Paul Kimiti na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo, Mizengo Peter Pinda (Waziri Mkuu Mstafu), wametoka misaada ya Sabuni za unga na Vipande, Mafuta ya Kupakaa, Miswaki Dawa Meno Pamoja na Juisi katika Gereza la Utete Rufiji, Mkoani Pwani..

Amesema, Misaada hiyo ilikuwa inalenga kusherekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,  kwa kuwalenga wafungwa na kuwaomba Wadau nchini wajitokeze kuwasaidia Wafungwa na mahabusu misaada mbalimbali kwani bado wanamahitaji.

Kwa Upande wa Mkuu wa Gereza la Utete, Christopher Mwenda Kwa niaba ya Mkuu wa Magereza Mkoa, amewashukuru Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Pwani namna wanavyoendelea kuwatia moyo wafungwa.

Naye Monica Mbilla,Mkuu wa idara ya Malezi ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Pwani, amesema Msaada Mkubwa atakao wasaidia kuhakikisha wanapewa elimu na Msaada wa kisheria.

Makala: Waziri wa dhiki na mipango ya ghafla
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 13, 2024