Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya England ‘The Three Lions’  Sven-Goran Eriksson, amesema amebakisha mwaka mmoja kuishi baada ya kugundulika kuwa na saratani isiyotibika.

Eriksson mwenye umri wa miaka 75, alikuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa England na aliiongoza nchi hiyo kufika Robo Fainali za Kombe la Dunia 2002 na 2006 na michuano ya Euro 2004.

“Ukipata meseji kama hiyo, unathamini kila siku na unafurahi unapoamka asubuhi na unajihisi sawa, kwa hiyo ndicho ninachofanya,” alisema Eriksson akikiambia Kipindi cha BBC World Sporting Witness.

Eriksson, ambaye amefundisha kabumbu kwa miaka 42, aligundulika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita na aliacha majukumu yake ya hivi karibuni ya ukurugenzi wa michezo katika klabu ya Karistad ya Sweden miezi 11 iliyopita kutokana masuala ya afya.

Klabu alizofundisha ni pamoja na Degerfors na Gothenburg za Sweden, Benfica ya Ureno, AS Roma, Fiorentina, Sampdoria na Lazio za ltalia na akitwaa mataji kadhaa.

Pochettino apotezea usajili Chelsea
Yves Bissouma: AFCON 2013 ni maalum kwangu