Mauricio Pochettino amepuuza mapendekezo wanayoamini kuwa Chelsea inahitaji kusajili mshambuliaji Januari hii na kupuuzia uvumi wa kutaka kumnunua Mshambuliaji wa Brighton, Evan Ferguson.
Chelsea wametatizika kutafuta mabao msimu mzima na hawakuwa na Christopher Nkunku na Nicolas Jackson wakati wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fulham juzi Jumamosi (Januari 13) kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Pochettino alisema ljumaa kwamba “Tutaona hali ilivyo” baada ya kukiri wasiwasi wake kutokana na kudorora kwa hivi punde zaidi kwa Nkunku.
Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 52 kutoka RB Leipzig majira ya joto, ameichezea klabu hiyo mara nne pekee baada ya kupata jeraha baya la goti wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
Vyanzo viliiambia ESPN kwamba Chelsea inavutiwa na Victor Osimhen wa SSC Napoli na Ivan Toney wa Brentford, lakini uwezekano wa kuwasajili Januari hii ni mdogo.
Santiago Gimenez wa Feyenoord ni chaguo jingine, lakini alipoulizwa haswa kuhusu nia kwa Ferguson, Pochettino alisema: “Hapana, nadhani unajua vizuri sizungumzi kuhusu uvumi.
“Sitazungumza kamwe kuhusu wachezaji ambao wako katika klabu tofauti, naheshimika sana hapana hatuongei tunapima kikosi na ikitokea kitu tutawasiliana, lakini kwa sasa hatukuchukua maamuzi yoyote.
“Sijawahi kusema tunahitaji mshambuliaji wa kati. Hapana, kwa sababu baada ya hapo tunatengerneza tatizo, mimi na watu wangu. Sikuwahi kusema hivyo.
Sikusema hivyo jana katika mkutano wangu na waandishi wa habari kwamba tunahitaji mshambuliaji.