Katika kutekeleza Kampeni ya Mama Samia Ligal Aid, Taasisi zinazotoa huduma za Kisheria zimetakiwa kuungana na kuona ni kwa namna gani zinaweza kutoa msaada wa huduma ya kisheria bure kwa Wananchi ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba kila mwananchi anafahamu masuala ya kisheria.

Waziri wa Katiba na Sheria, Pindi Chana amesema hayo leo hii leo Januari 15, 2024 aliposhiriki kikao cha bodi ya Taifa ya Msaada wa Kisheria Jijini Dar es Salaam.

Amesema “tunaendeela kumshuruku Mhe. Rais wetu kwa maono haya makubwa ya Mama Samia Legal Aid Campaign kwani tunaposema huduma hii ifanyike bila malipo ni azma ya Mhe. Rais kwamba Wananchi wapate huduma hii bure.’’

“Ni Mhe Rais ameamua kuhakikisha kwamba anawezesha na kuchangia ili Wananchi waweze kusikilizwa na kutoa hoja zao na kuelekezwa yale yanayowapasa, Rais wetu ameweka fungu maalum katika bajeti ambayo imepitishwa na Bunge, ametupa maelekezo thabiti kabisa, nendeni kwa Watanzania mkawasikilize hoja zao, hilo Mhe. Rais ameamua analigharamia kikamilifu kabisa,’’ alisisitiza Chana.

Aidha, amesema Wizara ya katiba na Sheria inaenda kuandaa mwongozo maalum ambao utaonyesha ni wapi wanasheria wanatoa huduma ya kisheria bure katika kila Mkoa na kila Wilaya, hivyo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampeni hiyo ambayo lengo ni lake ni kufika katika Mikoa yote ambapo kwa sasa ipo Mkoani Singida katika siku yake ya tano Mkoani humo, Halmashauri zote, kata 70 na Vijiji 2012 vinatarajia kunuifaka na kampeni hiyo.

Kenya Airways marufuku Tanzania - TCAA
Majaliwa angoza kikao Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050