Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Dkt. Abdulaziz Abood amefanya ziara ya kushutukiza kwenye Kata ya Mazimbu kwa lengo la kujionea Miundombinu ya Barabara zilivyo, kwa kipindi hiki cha mvua.

Akiwa maeneo ya Barakuda huko Kata ya Mazimbu, Dkt. Abood amejionea ubovu wa barabara hiyo inayoelekea chuo Kikuu cha Kilimo – SUA, Kampasi ya Mazimbu kwa jinsi ilivyoaribiwa na mvua zinazoendelea.

Sababu za kuaribika kwa barabara hiyo ni maji yanayopita Mto Ngerengere kuacha mkondo wake na kukatisha kwenye barabara hiyo, jambo ambalo linasababisha watumiaji wa barabara hiyo kuvuka kwa shida na pia ni  hatari kwa afya za W ananchi.

Aidha, kutokana na adha hiyo Mbunge Abood ameahidi kuongea na TARURA ili kufanya haraka kurekebisha barabara hiyo na kuzuia mikondo ya maji yanayoelekea katika makazi ya Wananchi, kukatisha kwenye Barabara sambamba na uchimbaji wa mitaro.

Mradi LTIP kuongeza usalama milki Ardhi Nchini
Msuva: Bado kuna alama sita AFCON 2023