Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP), ambao chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi unaotekelezwa nchini unalenga kupanga, kupima, kumilikisha na kutoa hati miliki za ardhi kuongeza usalama wa milki za ardhi.

Akiongea hivi karibuni jijini Dodoma, Mratibu Msaidizi wa Mradi huo, Dkt. Upendo Matotola amesema mradi huo unatumika kama mfano kwa ulimwengu na kuwasisitiza washiriki hao kuijenga nchi kwa pamoja, ili kuleta taswira njema ya Tanzania kimataifa.

Amesema, “tunajua kabisa tunapopanga, tunapopima, na kumilikisha vipande vya ardhi, Uchumi wetu unaongezeka kwa sababu ardhi iliyopangwa na kupimwa inaongezeka thamani na inapoongezeka thamani, shughuli za kiuchumi nazo zinaongezeka” amesema Dkt. Upendo.

Dkt. Upendo amesema, Serikali inatoa kipaumbele kwa sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kijamii katika kutekeleza masuala ya ardhi na kusisitiza kuwa Serikali itabaki na jukumu la kujenga uwezo, mazingira wezeshi, utawala na usimamizi wa ardhi nchini.

Kwa upande wao washiriki wa kikao kazi hicho, akiwemo Innocent Jaji na Mariam Mohamed wamesema Asasi za Kiraia zinajukumu la kushirikiana na Serikali katika kutelekeza mradi huo, kwa kutoa elimu ya masuala ya ardhi makundi maalumu wakiwemo wanawake, wazee, watoto na watu wenye ulemavu.

Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) ambao unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia umeanza mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika 2027 ambapo jukumu lake ni kurasimisha ardhi kwa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.

Benchikha kuzivutia kasi Azam, Young Africans
Mvua zamtembeza Mbunge Abood, avunja ukimya