Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo wa utendaji katika Sekta ya Ardhi nchini, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa utoaji huduma za sekta ya ardhi, ikiwemo Programu ya Kupanga, Kupima, Kumilikisha ardhi (KKK) kwa kushirikisha sekta binafsi na mamlaka za upangaji.

Kauli hiyo, imetolewa na Waziri wa Wizara hiyo, Jerry Silaa jijini Dar es salaam wakati wa kikao chake kuhusu siku 100 tangu alipoingia kuhudumu ofisi hiyo alipoteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema yatafanyika marekebisho ya utaratibu wa kukopesha fedha kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Viwanja utakaokuwa unatunza fedha na kukopesha fedha kwa ajili ya programu hiyo.

Amesema,“Wizara inakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo wa utendaji katika Sekta ya Ardhi nchini ambayo yanalenga kuboresha utendaji kazi katika utoaji huduma za sekta ya ardhi,

Aidha, Silaa ameongeza kuwa Wizara pia inakamilisha maboresho ya mfumo wa TEHAMA ambao utaruhusu huduma na miamala ya sekta kuanza kutolewa kidigitali utakaoanza kutumika hivi karibuni na kwamba walizindua rasmi mfumo wa ARDHI KLINIKI KIGANJANI maalumu kwa kupokea na kushughulikia malalamiko yatakayowasilishwa.

Young Africans kushusha mtu kazi
Wengine kusimamishwa Simba SC