Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa ni mwendo wa kazi ndani ya timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku wakilenga kufanya vizuri kutokana na uimara wa kikosi chao.

Young Africans ina majembe mapya matatu ambayo ni Augustine Okrah, Shekhan Ibrahim na Joseph Guede.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe alisema kuwa wanatanmbua ushindani uliopo, hivyo uwepo wa wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi kitaongeza nguvu na tabu kwa wapinzani.

“Kazi kubwa itakuwa kwenye ushindani kimataifa na kitaifa tunajua kwamba ushindani ni mkubwa lakini kwa namna ya wachezaji tuliona wapinzani watapata tabu hapa kwetu kazi tu. Kila mmoja anatambua kwamba ushindani ni mkubwa kazi ipo.

Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zilizopo na muda upo kwa ajili ya maandalizi yanayofuata kitaifa na kimataifa, kwa kuwa ushindi unapatikana uwanjani kwa wachezaji kujituma na kufanya kazi yao kuwapa burudani mashabiki ndani ya uwanja,” amesema Kamwe.

Kidunda: Kisasi kitalipwa kwa Asamahle
Makala: Mtihani wa Maji uliozua utata kichawi