Uchawi.

Uchawi ni kitendo kinachofanywa na watu wanaofanya uchawi, wakitumia vitu vya asili kutimiza haja zao ili wapate msaada au kuleta mabadiliko ya jambo fulani na pia hutafsiriwa kama nguvu zisizo za kawaida za kuwadhuru au kuwaadhibu wengine.

Wachawi wengi zamani walifikiriwa kuwa ni wapagani wanaofanya kazi ya Ibilisi lakini hata hivyo wengi wao walikuwa ni Waganga wa asili au wale wanaoitwa “wazee wenye busara” ambao uchaguzi wao wa taaluma haukueleweka na haijulikani ni lini hasa uchawi ulianza kihistoria, lakini mojawapo ya rekodi za mapema zaidi za mchawi ziko katika Biblia katika kitabu cha 1 Samweli, kinachofikiriwa kuwa kiliandikwa kati ya 931 K.K. na 721 B.K.

Aya katika kitabu hicho inasimulia hadithi ya wakati Mfalme Sauli alipomtafuta Mchawi wa Endori kuita roho ya nabii Samweli aliyekufa, ili kumsaidia kushinda jeshi la Wafilisti. Mchawi huyo alimwamsha Samweli, ambaye kisha akatabiri kifo cha Sauli na wanawe. Siku iliyofuata, kulingana na Biblia, wana wa Sauli walikufa vitani, na Sauli akajiua.

Mistari mingine ya Agano la Kale inashutumu wachawi, kama vile Kutoka 22:18 inayotajwa mara nyingi, “usimwache mchawi kuishi” na hata hivyo vifungu vya ziada vya Biblia vinaonya dhidi ya uaguzi, kuimba au kutumia wachawi kuwasiliana na wafu.

Mshtuko wa Uchawi.

Ulitawala Ulaya katikati ya miaka ya 1400, wakati wachawi wengi walioshtakiwa walikiri (mara nyingi walipopata mateso), kwa aina mbalimbali za tabia mbaya, ambapo katika muda wa karne moja, matukio ya uchawi yalikuwa ya kawaida na wengi wa washtakiwa waliuawa kwa kuchomwa kwenye mti au kunyongwa na katika hili, Wanawake wasio na waume, wajane na wanawake wengine walio pembezoni mwa jamii ndio hasa walilengwa.

Kati ya miaka ya 1500 na 1660, hadi watu 80,000 walioshukiwa kuwa wachawi waliuawa huko Uropa na asilimia 80 kati yao walikuwa wanawake waliofikiriwa kuwa katika urafiki na Ibilisi na waliojawa na tamaa, huku ikiarifiwa kuwa Ujerumani ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha mauaji ya wachawi, wakati Ireland ilikuwa na kiwango cha chini zaidi.

Kuchapishwa kwa kitabu “Malleus Maleficarum” kilichoandikwa na Wadominika wawili wa Ujerumani walioheshimika sana mwaka wa 1486, kulichochea matukio ya uchawi na yakaenea kwa kasi. Kitabu hicho, ambacho kwa kawaida kilitafsiriwa kama “Nyundo ya Wachawi,” kilikuwa mwongozo wa jinsi ya kutambua, kuwinda na kuhoji wachawi.

Hata hivyo, “Malleus Maleficarum” iliita uchawi kuwa ni uzushi, na kwa haraka ikawa mamlaka kwa Waprotestanti na Wakatoliki wanaojaribu kuwaondoa wachawi wanaoishi kati yao. Kwa zaidi ya miaka 100, kitabu hicho kiliuza nakala nyingi zaidi za kitabu kingine chochote katika Ulaya isipokuwa Biblia.

Uchawi wa Salem.

Taratibu hali ya wasiwasi wa uchawi ilipungua huko Uropa, ilikua ni katika Ulimwengu mpya ambao ulikuwa unakabiliwa na vita kati ya Wafaransa na Waingereza, hofu iliyoendelea ya kushambuliwa na makabila ya asili ya Amerika na majanga mbalimbali yalihitaji Mbuzi wa Azazelim, ambapo hapo majaribio ya wachawi yanayojulikana sana yalifanyika Salem, jimbo la Massachusetts mwaka 1692 Nchini Marekani.

Majaribio ya uchawi wa Salem yalianza wakati Elizabeth Parris (9) na Abigail Williams (11) walipoanza kuteseka na kutokwa na damu, michirizi ya mwili na kupiga kelele bila kudhibitiwa (leo, inaaminika kuwa walikuwa na sumu kuvu ambayo ilisababisha spasms na kuwapa madhara).

Wanawake wachanga zaidi walipoanza kuonyesha dalili hali ya wasiwasi ilianza na wanawake watatu walishtakiwa kwa uchawi: Sarah Good, Sarah Osborn na Tituba, Mwanamke mtumwa aliyemilikiwa na baba yake Parris. Hata hivyo, Tituba alikiri kuwa yeye ni mchawi na akaanza kuwashutumu wengine kwa uchawi.

Badaye, Askofu Bridget akawa mchawi wa kwanza aliyeshtakiwa na kuuawa wakati wa Majaribio ya Wachawi wa Salem alipotundikwa kwenye mti wa Salem. Hatimaye karibu watu 150 walishtakiwa na 18 waliuawa. Wanawake hawakuwa wahasiriwa pekee wa Majaribio ya Wachawi wa Salem kwani wanaume sita pia walitiwa hatiani na kunyongwa.

Massachusetts haikuwa ya kwanza kati ya makoloni 13 yaliyohangaikia uchawi, ingawa huko Windsor, Connecticut mnamo 1647, Alse Young alikuwa mtu wa kwanza katika Amerika kunyongwa kwa kujihusisha na uchawi na kabla ya kesi ya mwisho ya uchawi ya Connecticut kufanyika mwaka wa 1697, watu arobaini na sita walishtakiwa kwa uchawi katika jimbo hilo na 11 waliuawa.

Hata hivyo, huko Virginia watu hawakuwa na wasiwasi mwingi kuhusu wachawi na katika Kaunti ya Lower Norfolk mwaka wa 1655, sheria ilipitishwa na kuifanya kuwa uhalifu kumshtaki mtu kwa uwongo kwa uchawi lakini bado, uchawi ulikuwa ni jambo la wasiwasi huku majaribio ya wachawi yapatao dazeni mbili (zaidi ya wanawake) yakifanyika Virginia kati ya mwaka 1626 na 1730.

Je, Ni kweli Uchawi upo?

Mmoja wa wachawi maarufu katika historia ya Virginia, Grace Sherwood ambaye majirani zake walidai kuwa aliwaua nguruwe wao alifikishwa mahakamani mwaka wa 1706, hapo Mahakama iliamua kutumia mtihani wa maji uliozua utata, ili kubaini hatia au kutokuwa na hatia.

Mikono na miguu ya Sherwood ilifungwa na kutupwa ndani ya maji wakisema ikiwa atazama basi hatakuwa na hatia ila ikiwa alielea, alikuwa na hatia. Sherwood hakuzama na alihukumiwa kuwa mchawi lakini hata hivyo hakuuawa bali alifungwa gerezani na kwa miaka minane.

Nakala ya kejeli (inayodaiwa imeandikwa na Benjamin Franklin), kuhusu kesi ya wachawi huko New Jersey ilichapishwa mwaka 1730 kwenye Gazeti la Pennsylvania. Ilidhihirisha ujinga wa baadhi ya shutuma za uchawi na sheria zilipitishwa ili kusaidia kulinda watu kutokana na kushtakiwa vibaya na kuhukumiwa.

Kitabu cha Shadows.

Wachawi wa kisasa wa Ulimwengu wa Magharibi bado wanatatizika kutikisa mtindo wao wa kihistoria. Wengi wao hufuata Wicca ambayo ni dini rasmi nchini Marekani na Canada, yenyewe huepuka uovu na kuonekana kwa uovu kwa gharama zote. Kauli mbiu yao ni “kutomdhuru yeyote,” na wanajitahidi kuishi maisha ya amani, uvumilivu na usawa kulingana na maumbile na ubinadamu.

Wachawi wengi wa ki-siku-hizi bado hufanya uchawi, lakini mara chache huwa kuna jambo lolote baya kuwahusu. Uchawi wao mara nyingi unatokana na Kitabu chao cha Shadows, mkusanyo wa hekima na uchawi wa karne ya 20 na unaweza kulinganishwa na tendo la maombi katika dini zingine. Dawa ya kisasa ya uchawi ina uwezekano mkubwa wa kuwa dawa ya mitishamba kwa mafua badala ya hex kumdhuru mtu.

Uchawi wa siku hizi kwa kawaida hutumiwa kumzuia mtu asifanye maovu au kujidhuru. lakini Ajabu ni kwamba yawezekana baadhi ya wachawi wa kihistoria walitumia uchawi kwa makusudi kutenda maovu, huenda wengi waliukubali kwa ajili ya uponyaji au ulinzi dhidi ya ubaya walioshutumiwa.

Lakini Uchawi, iwe ni wa kweli au ni tuhumiwa bado unakabili manyanyaso na kifo. Wanaume kwa Wanawake kadhaa wanaoshukiwa kutumia uchawi wamepigwa au kuuawa nchini Papua New Guinea tangu 2010, akiwemo mama mdogo aliyechomwa moto akiwa hai.

Matukio kama hayo ya ukatili dhidi ya watu wanaodaiwa kuwa wachawi, yametokea barani Afrika, Amerika Kusini, Mashariki ya Kati na katika jumuiya za wahamiaji barani Ulaya na Marekani.

Young Africans imedhamiria 2023/24
Manchester City yashtukia jambo