Takriban kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Gambia, Banjul hapo utakuwa umefika katika Vijiji vidogo vya Kitamaduni vya Jufureh na Albreda.

Vijiji hivyo, wanaishi watu wa jamii ya Wolof na Mandinka na eneo hilo lilitimika kwa biashara ya utumwa kwa karne nyingi na mapigano kati ya Mataifa ya Ulaya wakigombea kudhibiti wa Mto Gambia.

Ni hapa hapa ambapo uzao wa Kunta Kinteh bado unaishi, tena kwenye vibanda vya jadi na kukiwa na urithi wa mabaki ya kikoloni, hivyo kufanya kuwa eneo la kihistoria.

Mtu huyu mweusi mgumu (Kunta Kinte), aliwahi kuhusishwa kwenye riwaya ya ‘Roots’ ya mwaka 1976, iliyokuwa imebeba maudhui ya madhila na biashara ya utumwa.

Mwandishi Mmarekani, Alex Haley, anatuambia kuwa filamu hiyo ambayo Kunta Kinte alikuwa ni muhusika mkuu, ni msingi wa hadithi ya kweli ya maisha wakati wa enzi za mababu.

Ipo hivi, kuna Meli ya watumwa iitwayo Lord Ligonier, iliyokuwa ikisafiri kutoka Mto Gambia, Julai 5, 1767, ikiwa na Wagambia 140 waliotekwa na ilifika Annapolis, Maryland Septemba 29, 1767, ikiwa na manusura 98 pekee.

Haley anaamini kwamba mmoja wa watu  walionusurika alikuwa ni Kunta Kinte mwenye umri wa miaka kumi na saba kwa wakati huo nankisha waliuzwa utumwani Oktoba 7, 1767.

Kunta Kinte kama alivyoigizwa na mwigizaji LaVar Burton, alinunuliwa ili kutumikishwa kwenye meli au katika moja ya nyumba za wageni au mikahawa ya ndani.

Kisha alipelekwa kwenye shamba huko Virginia ambako aliendeleza harakati zake za kupambania kujikomboa toka kwa watwana.

Hata hivyo, kuwasili kwa Kinte huko Annapolis ni ishara ya enzi ya biashara ya utumwa kufuatia mamilioni ya Wanaume, Wanawake na watoto wa Kiafrika kitekwa na kutumikishwa.

Walistahimili hali ya kutisha ya “Njia ya Kati” – kivuko cha Atlantiki ambamo Waafrika walijaa kwenye sehemu za meli kwa miezi kadhaa, huku wengi wakifa njiani.

Kunta Kinte alizaliwa mwaka 1750, katika jamii hiyo ya watu wa kabila la Mandika nchini Gambia akiwa ni miongoni mwa watumwa waliosafirishwa na kupelekwa Amerika katika zama za Biashara ya utumwa kwa kuvuka Bahari ya Atlantiki.

Kunta ni mzaliwa toka ukoo wa kinte, ambayo inaheshimika zaidi katika kabila la Mandika wa huko nchini Gambia.

Alikuwa ni shujaa msomi, mwerevu, mwenye ujuzi na shupavu, mwenye ujasiri ambao ulimsaidia alipokuwa akikamatwa na Wafanyabiashara ya utumwa.

Katika siku zote alizokuwako huko utumwani Amerika, Kunta Kinte hakuwahi kukata tamaa ya kurejea nyumbani kwao Gambia.

Alikuwa pia ni kinara wa kuwahamasisha na kuwapatia ujasiri watumwa wenzake kupigania uhuru wao na hatimaye wengi waliweza kupambana na kufanikiwa kujikomboa.

Licha ya kwamba alifariki dunia mwaka 1822, lakini mawazo yake bado yanaishi mpaka leo.

Waliosajiliwa dirisha dogo Tanzania Bara
Jaji Mkuu alitahadharisha Taifa, amuandikia barua Rais