Sina shaka unaifahamu ama ushawahi kuiona mistari inayogawa Barabara iliyonakshiwa na rangi nyeupe ama katikati au pembeni ya Barabara.

Chapisho kutoka ukurasa wa Mabalozi wa Usalama Barabarani – RSA, linaeleza kuwa Edward N. Hines, raia wa Marekani aliyezaliwa 1870 na kufariki 1938 ni mmoja wa Wataalamu ambao waliochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya miundombinu ya barabara.

Inaarifiwa kuwa, moja kati ya mambo ambayo aliyabuni ni mstari mweupe unaogawa barabara katikati. Lakini cha kufurahisha zaidi na ambacho pengine hukijui ni kuwa, ugunduzi huo wa Hines, ulichagizwa na gari la maziwa.

Inaelezwa katika eneo alikokuwa akiishi Hines, kulikuwa na gari ya kusambaza maziwa iliyokuwa ikipita hapo kila siku, lakini gari hiyo ilikuwa ikivujisha maziwa kwakuwa tanki lake lilikuwa na hitilafu.

Maziwa hayo yaliyokuwa yakimwagika, yalitengeneza mstari mweupe ambao Hines, aliona unafaa kutumika kugawanya pande mbili za barabara badala ya hali ilivyokuwa awali ambapo madereva walikuwa wanatakiwa kila mmoja kubana upande wake.

Hines akaliweka wazo hilo katika mkakati na kulifanyia kazi na huo ukawa mwanzo wa mstari mweupe unaogawa barabara, ingawa baadae kuna maeneo walipendekeza kutumia mstari wa njano.

Makala: Mwamba wa 'The God Must Be Crazy' aliamka
Jenerali agomea upatanisho, adaiwa kutaka vifo zaidi